Msaada wa Kikwete kwa FDLR, je anajua madhara yake Kwa Tanzania na eneo zima?

By Mamdani Githongo
0

Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Uadui, chuki, uchokozi na fitina vyaonekana wazi katika maneno na mipango ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania; waziri wake wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa bwana Bernard Membe kiasi kwamba yuko hatarini ndani ya Tanzania na nchi majirani.

Tafsiri ya Kikwete juu ya kundi la magaidi hatari la FDLR, maelezo ambayo bwana Membe anayaimba mbele ya jumuia ya kimataifa kila siku ni hadaa tupu.

Wao wanatulaghai bila woga kwamba FDLR waliopo leo ni watoto na hawajahusika na mauaji ya halaiki ama ya kimbari ya watutsi zaidi ya milioni moja huko Rwanda mwaka 1994. Kikwete anawatetea na kusema waliofanya hayo masaibu wamo kundini lakini sio kundi lote lakini anajua vizuri sera ya FDLR na falisafa yao kama kundi.

Tafsiri halisi ya hawa wauaji mnaowaita watoto ni kurudisha utawala wakihutu nchini Rwanda ambao lengo kuu ni kumalizia kazi ambayo walitamani kukamilisha lakini wakagonga mwamba baada ya kukatizwa na utawala uliopo madarakani hivi sasa. Kundini wamo wakongwe wakufunzi wa FDLR ambao tayari wamewalisha sumu ya fikra mbovu hao ambao Kikwete na Membe wanawaita watoto bila kujua itikadi ndio silaha yao kuu.

Wamelishwa chuki na damu kwa itikadi ndio maana wanang’ang’ana kuendeleza mauaji ya kimbari. Wasipozuiwa wataendeleza hizo itikadi zao mbovu hadi ukanda wote wa maziwa makuu na Tanzania tumo kundini!

Kikwete amekuwa kama mlevi anaye yumba kutafuta pakujishikiza na asipate. Amekuwa akigonga huku na huko ilimradi asianguke lakini dalili zinaonesha kuwa anguko lake litakuwa kubwa kama Mheshimiwa/waheshimiwa hawa wameonesha wazi mapenzi yao ya dhati na huruma kwa kundi la maharamia na magaidi  wa  FDLR, watu ambao Umoja wa mataifa una watafuta kwa kuhusika moja kwa moja na mauaji ya Kimbari ya Watutsi zaidi ya million moja huko Rwanda mwaka 1994.

Pamoja na hayo, hapa nchini Tanzania kumekuwa na manung’uniko na vilio kila kukicha kiasi kwamba watanzania hatuko salama tena katika nchi hii ambayo Muasisi wake Hayati Mwalimu Kambarage Nyerere, warithi wake Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamin William Mkapa waliiweka katika hari ya usalama hata wengi wetu kuiona Tanzania yetu hii kama kisiwa kikubwa cha amani.

Dhoruba ya ufisadi, Mabomu; Katiba na Gesi

Kama wasemavyo waswahili, mwenye macho haambiwi tazama. Mkoa wa Arusha ambao ni mkoa wa kwanza kwa utalii nchini Tanzania hasa kabla ya kuugawa katikati na kuzaa mkoa mpya wa Manyara, sasa watalii bora waende Somalia kuliko Arusha ambako kila leo mabomu huuwa watu na kuwafanya wengi vilema wa maisha.

Wanalipuliwa watu katika Mihadhara ya vyama vya upinzani hasa kile cha CHADEMA, Makanisani wakristo wanauawa kwa mabomu hata hawajali kukiwa na askofu ama mjumbe kama Balozi wa Baba mtakatifu; wanalipua tu.

1

Moja ya mlipuko uliotokea katika kanisa Katoliki Arusha: Pichani ni Masista wakikimbia kuokoa maisha yao, waumini waliozirai na majeruhi waki gaagaa chini bila msaada

Huyu jamaa anaejifanya mwana diplomasia hataki kuzungumza na wapinzani wake ama wenye mawazo tofauti naya kwake bali ana amua kuwalipua na kusingizia magaidi. Waandishi wa habari nao wameuawa, wameteswa na kufungiwa wanaposema ukweli kuhusu hari halisi nchini.

Tanzania ina Radio Stations 86 na TV 28 zilizosajiliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), na jumla ya magazeti zaidi ya 300 ambayo yamesajiliwa na idara ya habari maelezo lakini imekuwa katika nchi zinazo fanya vibaya sana katika tasinia ya habari pamoja na rundo hili la  taasisi za habari tena zilizo sajiliwa.

Raisi Kikwete amesikika akisema kama wajumbe wa bunge la katiba watapitisha serikali tatu,uchaguzi wa serikali za mtaa hautakuwepo mwaka huu,kwani itabidi usubiri katiba ya Tanganyika,Mh Raisi hapa kaongopa. Jaji WARIOBA alisema kama katiba mpya itapita,haitaanza kutumika sasa,itaanza kutumika baada ya miaka minne ili kupisha marekebisho ya sheria ndogondogo hivyo uchaguzi hauwezi kuathirika na mabadiliko yoyote ya katiba.

Siri ya Sakata la Gesi na mikataba ya kugushi

Mkataba wa siri wa uchimbaji wa Gesi umevuja,haieleweki namna mapato yatakavyogawanywa kati ya serikali ya kampuni ya Statoil ya Norway iliyopewa tenda ya kuchimba gesi huko Mtwara. Kwa majibu wa mkataba huo,mgawanyo huo wa mapato utasababisha Tanzania kupata hasara ya shilingi Trilioni 1.6. kila mwaka,hasara hii ni kwa kitalu namba mbili tu.

Tanzania inatajwa kuwa na kiasi cha gesi asilia trilioni 20,sawa na mapipa bilioni 4 ambacho ni kiwango zaidi ya mafuta yaliyogunduliwa katika nchi za Uganda na Ghana kwa pamoja.

Ndani ya kipindi cha miaka 15 ambacho kampuni ya Statoil kutoka Norway itachimba gesi kwenye kitalu namba mbili,watajikusanyia kiasi cha dola za marekani bilioni 5.6.  Toka Tanzania ipate Uhuru miaka 51 iliyopita,imepatiwa misaada yenye thamani ya dola za marekani bilioni 2.5,lakini wahisani wanafiki hawa wakiwa na uhakika wa kukusanya dola bilioni 5.6 ndani ya miaka 15. Kikwete anayajua yote haya vizuri japokuwa anafumbia macho makusudi

Awali serikali ilisema kuwa kwenye sekta ya gesi,serikali na mwekezaji wangegawana  asilimia 50 ya mapato,lakini kwa mujibu wa mkataba huo wa gesi kati ya serikali na statoil,mwekezaji atapata asilimia 70 ya mapato huku serikali ikiambulia asilimia 30 tu,kwenye mapato hayo ya gesi.

Mchanganuo huu,ni kwa mujibu wa mkataba wa gesi kati ya serikali na statoil ya Norway uliovuja hivi karibuni na kusambazwa mitandaoni

Kufikia sasa, Kikwete hana sera wala hajaweka sheria, hajaandaa,teknolojia na kumasoko kusaidia uvunaji mzuri wa kiwango cha gesi kilichogundulika nchini ambacho mpaka sasa utafiti unaonesha gesi iliyogunduliwa ina thamani ya dola za kimarekani Bilioni 960.  Ripoti ya shirika la fedha ulimwenguni  (IMF) inaeleza kuwa uzalishaji wote wa gesi nchini Tanzania utaipatia Tanzania kiasi cha kati ya dola bilioni 3 mpaka 6 kwa mwaka.

Sikiliza Kikwete, Watanzania hatutaki vita

Wakati Rais Kikwete alipokuwa akihutubia umati wawatu na wanajeshi siku ya mashujaa Tanzania mwezi wa saba mwaka jana, alijigamba kusema Tanzania itapigana kuilinda mipaka yake kwa gharama yoyote. Watanzania tumesema mara nyingi na tunarudia:

Hatutaki vita na wala huyu Mkwere asituletee mzaha maana katika ugomvi wake sisi watanzania hatumo.

“Wale wote watakao jaribu kuivamia nchi yetu watakiona cha mtema kuni. Nchi yetu iko salama na wanajeshi wetu wako makini” Alionya Kikwete.

Nani kamwambia tunahaja na vita ama tuna ugomvi na nchi yoyote? Labda hawa watoto wake alowazaa kisiasa na kijamaa zaidi kwa siri, hawa hawa walio leta majanga huko Rwanda mwaka 1994, nazungumzia hawa waasi wa FDLR.

Inaonekana kama ataendelea kuwaenzi na kuwanyonyesha yatamtokea puani. Wale jamaa wamenawa damu za mamilioni ya watu wasio na hatia, waasi wenye mikosi kama wale sijui Bwana Kikwete anahangaika nao nini. Ama kweli kama ilivyo wahi kuvuma huenda jamaa ni ndugu yao.

Ukweli ni kwamba tunafumbwa macho

Haya makinda makinda anayotuchezea Kikwete yana siri moja, baada ya kuona nchi imemshinda, wapinzani wamekuwa wakali na amewekwa kiti moto na katiba mpya ambayo UKAWA wameikimbia; jamaa anahaha.

Ufisadi wa kila aina, milipuko ya hapa na pale na sintofahamu ya kuyumba kwa sekta muhimu kama elimu na afya vinamfanya Kikwete atafute sehemu ya kuhamishia fikra za Watanzania. Anataka wawaze na kupanga vita ili wasahau matatizo ya ndani ya nchi.

Ugomvi wa Kikwete na nchi za Malawi,Rwanda hauna msingi wowote hasa baada ya kugundulika kuwa sisi kama watanzania tumegoma kumuunga mkono. Inashangaza kuwa Kiongozi mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu kama Kikwete haoni ama anapuuza maoni yetu wananchi na hata wabunge wetu. Ulingoni amebaki yeye na waziri wake wa mambo ya njye na ushirikiano wa kimataifa bwana Bernard Membe.

Malawi imewashinda wakahamia Rwanda kwa mtindo wa kujifanya wafadhili wa kundi la kigaidi la FDLR.

Kikwete na Membe wameshindwa kuitumia hii diplomasia yao ndani ya nchi hapa hapa Tanzania, nje ya mipaka  wataweza? Wana majibu gani kwa familia zetu hasa sisi tuliopoteza watu wetu ndani ya jeshi letu wakipigania wasicho kijua, wakilala njaa porini kutetea maslahi ya tumbo na matakwa ya mtu mmoja kama Kikwete? Wanajeshi wanaoshindwa kutulinda hapa mkoani Mara tunapo uana ovyo, hapa Arusha tukilipuliwa, hapa Mtwara tukiporwa na Nyasa tukidhurumiwa wanauawa Congo kwa faida ya nani.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s